عن أبي هريرة رضي الله عنه:
أَنَّ رَجُلًا قَالَ لِلنَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَوْصِنِي، قَالَ: «لَا تَغْضَبْ» فَرَدَّدَ مِرَارًا قَالَ: «لَا تَغْضَبْ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6116]
المزيــد ...
Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Ya kwamba mtu mmoja alisema kumwambia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Niusie, akasema: " Usikasirike" Akarudia mara kadhaa, akasema: "Usikasirike".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6116]
Mmoja kati ya Masahaba -Radhi za Allah ziwe juu yao- alimuomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amjulishe katika jambo litakalomnufaisha, akamuamrisha asikasirike, na maana ya hapa nikuwa aziepuke sababu zinazoweza kumpelekea katika kukasirika, na aidhibiti nafsi yake na hasira zinapompata, asiendelee na hasira zake mpaka kufikia kuuwa au kupiga au kutoa matusi na mfano wa hayo.
Na yule bwana akarejea tena kuomba usia mara kadhaa, hakumzidishia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika usia zaidi ya "Usikasirike"