عن المِقدام بن معدي كرب رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«إِذَا أَحَبَّ الرَّجُلُ أَخَاهُ فَلْيُخْبِرْهُ أَنَّهُ يُحِبُّهُ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في الكبرى وأحمد] - [سنن أبي داود: 5124]
المزيــد ...

Imepokelewa Kutoka kwa Mikidadi bin Ma'di Yakrib -Radhi za Allah ziwe juu yake- Kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapompenda mtu ndugu yake basi na amueleze kuwa anampenda".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Abu Daud, Tirmidhiy na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ahmad] - [Sunanu Abii Daud - 5124]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- moja ya sababu ambazo hutia nguvu mahusiano kati ya waumini na hueneza mapenzi baina yao, nako ni kuwa mtu atakapompenda ndugu yake basi na amueleze kuwa anampenda.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa mapenzi ya dhati yanayokuwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, si kwa ajili ya masilahi ya kidunia.
  2. Inapendeza na ni sunna kumueleza anayependwa kwa ajili ya Allah, ili kuongeza mapenzi na kuzoeana.
  3. Kuenea kwa mapenzi baina ya waumini hutia nguvu udugu wa kiimani na huhifadhi jamii kuto pasuka na kufarakana.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (67)