+ -

عن أبي سعيد الخُدْريِّ رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«‌مَنْ ‌رَأَى ‌مِنْكُمْ ‌مُنْكَرًا فَلْيُغَيِّرْهُ بِيَدِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِلِسَانِهِ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبِقَلْبِهِ، وَذَلِكَ أَضْعَفُ الْإِيمَانِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 49]
المزيــد ...

Hadithi imepokelewa na Abii Said Alkhuduriy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- akisema:
"Yeyote miongoni mwenu atayeona jambo ovu na baya basi aliondoshe kwa mkono wake, ikiwa hawezi kuliondoa kwa mkono wake basi aliondoe kwa ulimi wake, na ikiwa hawezi kuliondoa kwa ulimi basi na alichukie kutoka moyoni mwake, na kuchukia moyoni ni udhaifu wa imani".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 49]

Ufafanuzi

Anatuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kuuondoa uovu, na uovu ni kila alilolikataza Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa kadiri ya uwezo, Hivyo basi ikiwa mtu atauona uovu basi ni wajibu juu yake kuuondosha kwa mkono wake ikiwa atakuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo. Ikiwa atashindwa kuondosha uovu kwa mkono wake basi na auondoshe kwa ulimi wake, kwa kumkataza mwenye kufanya uovu huo, na amueleze madhara ya uovu huo na amuongoze katika kheri badala ya kufanya shari hiyo. Basi ikiwa atashindwa hatua hii ya pili, basi auondoshe uovu kwa kuchukia moyoni mwake, kwa kuuchukia uovu huo, na aazimie moyoni mwake kuwa kama angekuwa na uwezo wa kuuondosha uovu huo angeuondosha, Na kuuondosha uovu kwa moyo ni katika kiwango dhaifu zaidi cha imani katika kuuondosha uovu

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Miongoni mwa faida za hadithi hii ni kuwa
  2. hadithi hii ni msingi katika kuweka wazi hatua na taratibu za kuuondoa uovu.
  3. Maamrisho ya kwenda hatua kwa hatua katika kukataza uovu, hatua zote hizo ni kwa mujibu wa uwezo wa mtu.
  4. Kukataza uovu katika dini ni mlango mpana sana suala hilo hakuna wakulikwepa, na hulazimishwa kila muislamu kufanya hivyo kwa kadiri ya uwezo wake.
  5. Kuamrisha mema na kukataza mabaya ni katika mambo yanayofungamana na imani, na imani kwa kawaida huzidi na kupungua.
  6. Ni sharti katika kukataza uovu: kuwa na elimu ya kuwa kitendo hicho ni uovu.
  7. Ni sharti katika kuondoa uovu: Usipelekee kutokea uovu mkubwa kuliko huo.
  8. Kukataza uovu kuna taratibu zake na masharti ambayo anapaswa muislamu kujifunza.
  9. Kukataza maovu kunahitajia siasa ya kisheria, na kuwa na ujuzi na elimu.
  10. Kutokuondosha uovu kwa moyo ni dalili ya udhaifu wa imani.