عن معاوية رضي الله عنه قال: سمعت النبي صلى الله عليه وسلم يقول:
«مَنْ يُرِدِ اللهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ، وَإِنَّمَا أَنَا قَاسِمٌ، وَاللهُ يُعْطِي، وَلَنْ تَزَالَ هَذِهِ الْأُمَّةُ قَائِمَةً عَلَى أَمْرِ اللهِ، لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَالَفَهُمْ، حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 71]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Muawiya -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Mwenye kutakiwa kheri na Allah humpa ufahamu katika dini, mimi ni mgawaji tu, na Allah ndiye anayetoa, na umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka ije amri ya Mwenyezi Mungu".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 71]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mwenye kutakiwa kheri na Mwenyezi Mungu basi humruzuku ufahamu katika dini yake Mwenyezi Mungu Mtukufu, nakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ni mgawaji na msambazaji wa yale aliyopewa na Allah Mtukufu katika riziki na elimu na mengineyo, nakuwa mtoaji halisia ni Allah, na ama asiyekuwa yeye hao ni sababu tu hawawezi kunufaisha ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, nakuwa umma huu utaendelea kusimama katika amri ya Mwenyezi Mungu, hatowadhuru mwenye kuwapinga, mpaka Kiyama kisimame.