عن أبي هريرة رضي الله عنه قال:
سُئِلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنْ أَكْثَرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ الْجَنَّةَ، فَقَالَ: «تَقْوَى اللهِ وَحُسْنُ الْخُلُقِ»، وَسُئِلَ عَنْ أَكْثَرِ مَا يُدْخِلُ النَّاسَ النَّارَ فَقَالَ: «الْفَمُ وَالْفَرْجُ».
[حسن صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 2004]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
"Aliulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu mambo yatakayowaingiza watu peponi kwa wingi, akasema: "Ni uchamungu na tabia njema", na akaulizwa kuhusu mambo yatakayowaingiza watu motoni kwa wingi akasema: "Mdomo na utupu".
[Ni nzuri na nisahihi] - - [سنن الترمذي - 2004]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sababu kubwa zinazowapeleka watu peponi ni mbili:
Uchamungu na tabia njema.
Uchamungu: Ni mtu kuweka kinga kati yako na adhabu ya Mwenyezi Mungu, nako ni kwa kufanya maamrisho yake na kuyaepuka makatazo yake.
Na tabia njema: Inakuwa kwa kukunjua uso na kutenda wema na nakujizuia na kero.
Na sababu kubwa zinazowaingiza watu motoni ni mbili nazo ni:
Ni ulimi na utupu.
ulimi miongoni mwa maasi yake: Ni uongo, kusengenya, kuchonganisha, na mengineyo.
Na utupu katika maasi yake: Ni zinaa na kulawiti na mengineyo.