عن أبي ذر رضي الله عنه قال: قال لي النبي صلى الله عليه وسلم:
«لَا تَحْقِرَنَّ مِنَ الْمَعْرُوفِ شَيْئًا، وَلَوْ أَنْ تَلْقَى أَخَاكَ بِوَجْهٍ طَلْقٍ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2626]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Dhari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alisema kuniambia mimi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Kamwe!, Usidharau chochote katika wema, hata kama ni kukutana na ndugu ukiwa na uso mkunjufu".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2626]
Amehimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kutenda wema, na mtu asiudharau hata kama utakuwa kidogo, na miongoni mwake ni ukunjufu wa uso kwa kutabasamu wakati wa kukutana, ni lazima kwa muislamu alipupie hilo; kwa sababu hujenga kuwa na ukaribu na ndugu yako muislamu na huingiza furaha kwake.