عن المقدام بن معدِيْكَرِب رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«أَلَا هَلْ عَسَى رَجُلٌ يَبْلُغُهُ الْحَدِيثُ عَنِّي وَهُوَ مُتَّكِئٌ عَلَى أَرِيكَتِهِ فَيَقُولُ: بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ كِتَابُ اللهِ، فَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَلَالًا اسْتَحْلَلْنَاهُ، وَمَا وَجَدْنَا فِيهِ حَرَامًا حَرَّمْنَاهُ، وَإِنَّ مَا حَرَّمَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَمَا حَرَّمَ اللهُ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 2664]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Mikdad Bin Maadi Karbi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Kwa hakika imefikia wakati ambao mtu atafikiwa na hadithi yangu akiwa amekaa kwenye tandiko lake na akisema: Hakika kitakachotuhukumu kati yetu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu hivyo tukikuta halali ndani yake tutaihalalisha na tukikuta ndani yake kuna haramu tutaiharamisha, na kwa hakika chochote alichokiharamisha Mtume wa Mwenyezi Mungu Rehema na amani ziwe juu yake ni kama alichokiharamisha Mwenyezi Mungu".
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2664]
Amefahamisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake kuwa umefika wakati kutakuwa na kundi la watu, mmoja wao atakuwa amekaa na kuegemea katika tandiko lake, inamfikia hadithi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na kusema: Kitakachotuamua kati yetu na nyie kwenye mambo yetu ni Qur'ani tukufu pekee ndiyo inatutosha, tukikuta ndani yake halali tunaifanyia kazi, na tukikuta ndani yake haramu tunajiepusha nayo. kisha akaweka wazi Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila kitu alichokiharamisha au kukikataza katika sunna zake basi mambo hayo hukumu yake ni kama alivyoharamisha Mwenyezi Mungu katika kitabu chake; kwa kuwa yeye ni mfikishaji kwa niaba ya Mwenyezi Mungu.