عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«مَا نَقَصَتْ صَدَقَةٌ مِنْ مَالٍ، وَمَا زَادَ اللهُ عَبْدًا بِعَفْوٍ إِلَّا عِزًّا، وَمَا تَوَاضَعَ أَحَدٌ لِلهِ إِلَّا رَفَعَهُ اللهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2588]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Sadaka haikuwahi kupunguza chochote katika mali, na hakuna jambo zuri zaidi analomzidishia Mwenyezi Mungu mja kwa kusamehe zaidi kama kupewa utukufu, na hakuwahi kunyenyekea yeyote kwa ajili Mwenyezi Mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu humnyanyua".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2588]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sadaka haipunguzi mali, bali inaikinga na maafa, na Mwenyezi Mungu humpa badala mwenye nayo ya kheri kubwa, inakuwa ni ziada na sio kupungua.
Na kusamehe kunapokuwa na uwezo wa kulipiza kisasi hakukuwahi kuzidisha kwa mwenye kusamehe isipokuwa nguvu na utukufu.
Na hakuwahi kunyenyekea na kujidhalilisha yeyote kwa kutaka radhi za Allah, si kwa kumuogopa yeyote, na si kwa kujipendekeza kwa yeyote, na wala si kwa kutaka manufaa kwake, isipokuwa mtu huyu malipo yake yatakuwa ni kunyanyuliwa na kupewa utukufu.