+ -

عن أبي بَكرة رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول:
«إِذَا الْتَقَى الْمُسْلِمَانِ بِسَيْفَيْهِمَا فَالْقَاتِلُ وَالْمَقْتُولُ فِي النَّارِ»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ هَذَا الْقَاتِلُ، فَمَا بَالُ الْمَقْتُولِ؟ قَالَ: «إِنَّهُ كَانَ حَرِيصًا عَلَى قَتْلِ صَاحِبِهِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 31]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Abii Bakra -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, basi muuaji na muuliwaji wote motoni" Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu huyu muuaji anaeleweka, na vipi kuhusu muuliwaji? Akasema: "Hata yeye alikuwa na pupa ya kumuuwa mwenzake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 31]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa wakikutana waislamu wawili kwa mapanga yao, akiwa na dhamira kila mmoja wao ya kummaliza mwenzake; Basi muuaji motoni kwa sababu ya kutekeleza mauaji ya kumuua mwenzake, Kuhusu muuliwaji, hilo likamtatiza Swahaba: Ni vipi anakuwa motoni? Akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa hata yeye pia anakuwa motoni kwa sababu ya pupa yake ya kumuua mwenzake, na hakikumzuia kuuwa zaidi ya muuaji kumuwahi na kummaliza.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Anastahiki adhabu mwenye kukusudia madhambi kwa moyo wake na akazifanya sababu zake.
  2. Tahadhari kali ya kutopigana waislamu kwa waislamu, na kuna ahadi ya moto.
  3. Mapigano kati ya waislam kwa haki hayaingii katika ahadi hii ya adhabu, mfano kama kuwapiga vita waasi na mafisadi.
  4. Mwenye kutenda dhambi kubwa hakufuru kwa kulifanya pekee; Kwa sababu Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kawaita wenye kupigana kuwa ni waislamu.
  5. Watakapokutana waislamu wawili kwa nyenzo yoyote miongoni mwa nyenzo za kuuwana, mmoja akamuunza mwenzake, basi muuwaji na muuliwaji wote motoni, na kutajwa panga katika hadithi ni sehemu ya mfano tu.