عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«قَالَ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ، مَنْ عَمِلَ عَمَلًا أَشْرَكَ فِيهِ مَعِي غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2985]
المزيــد ...
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2985]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa: Yeye amejitosheleza na uhitaji wa washirika wa kushirikishwa naye, Yeye ni tajiri wa kila kitu, na kuwa mwanadamu atakapofanya jambo katika ibada na akalifanya kuwa ni la Mwenyezi Mungu na mwingine asiyekuwa yeye, basi Allah humuacha na halikubali jambo hilo, na hulirejesha kwa mwenye nalo. Ni lazima kutakasa amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Yeye Mtukufu hakubali isipokuwa yale yatakayokuwa yametakaswa kwa kutaka radhi zake Yeye Mkarimu.