عن عبد الله بن عمرو رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«يقالُ لصاحبِ القرآن: اقرَأ وارتَقِ، ورتِّل كما كُنْتَ ترتِّل في الدُنيا، فإن منزِلَكَ عندَ آخرِ آية تقرؤها».
[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في الكبرى وأحمد] - [سنن أبي داود: 1464]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi Bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Ataambiwa msomaji wa Qur'ani: Soma na upande daraja, na soma kwa utulivu kama ulivyokuwa ukisoma Duniani, kwa hakika upandaji wa cheo chako utakomea katika Aya ya mwisho utakayoisoma."
[Ni nzuri] - - [سنن أبي داود - 1464]
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa msomaji wa Qur'ani mwenye kufanyia kazi yaliyomo ndani yake, aliyeshikamana na kuisoma na kuihifadhi, akiingia Peponi ataambiwa: Isome Qur'ani na upande cheo na daraja katika daraja za peponi, na usome kama vile ulivokuwa ukisoma Duniani kwa kuisoma kwa upole na utulivu; kwa hakika Cheo chako kitaishia kwenye Aya ya mwisho utakayo isoma.