عن أبِي هُرَيرةَ رضي الله عنه أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلمَ قال:
«إذا قُلْتَ لِصَاحِبِكَ: أَنْصِتْ، يومَ الجمعةِ، والْإِمامُ يَخْطُبُ، فَقَدْ لَغَوْتَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 851]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Utakapomwambia mwenzako: Nyamaza, siku ya Ijumaa, na imamu akihutubu, basi utakuwa umefanya mchezo".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 851]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa katika adabu za wajibu kwa atakayehudhuria hotuba ya Ijumaa: Ni kunyamaza na kumsikiliza hatibu; ili mtu azingatie mawaidha, nakuwa atakayezungumza walau kwa jambo dogo, na imamu akihutubu, akasema kumwambia mwenzie: "Nyamaza" na "Sikiliza", basi zitakuwa zimempita fadhila za swala ya Ijumaa.