عن عبد الله بن عمر رضي الله عنهما قال:
سَمِعَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلًا يَعِظُ أَخَاهُ فِي الْحَيَاءِ، فَقَالَ: «الْحَيَاءُ مِنَ الْإِيمَانِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 36]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake- amesema:
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- siku moja alimsikia mtu mmoja akimnasihi ndugu yake kuhusu haya (Aibu) akasema: "Haya ni katika imani".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 36]
Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alimsikia mtu mmoja akimnasihi ndugu yake aache kuwa na aibu sana! akambainishia kuwa haya ni katika imani, nakuwa huwa haiji ila kwa kheri.
Na haya ni tabia inayomsukuma mtu kufanya zuri na kuacha baya.