عن سَمُرَة بن جندبٍ رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«أَحَبُّ الْكَلَامِ إِلَى اللهِ أَرْبَعٌ: سُبْحَانَ اللهِ، وَالْحَمْدُ لِلهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ، وَاللهُ أَكْبَرُ، لَا يَضُرُّكَ بِأَيِّهِنَّ بَدَأْتَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2137]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Jundubi -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-
"Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lolote kati ya hao".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2137]
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa maneno yanayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ni manne.
Sub-haanallaah: Na hili linamaanisha kumtakasa Mwenyezi Mungu na kila aina ya mapungufu.
Na Al-hamdulillaah: Nako ni kumsifu Allah kwa ukamilifu uliotimia pamoja na kumpenda na kumtukuza.
Na Laa ilaaha illa llaah: Yaani: Hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Allah.
Na Allahu Akbaru: Yaani: Ni Mtukufu mno, na ni Mtakatifu mno kuliko kila kitu.
Nakuwa fadhila zake na kupata thawabu zake si lazima kuyapangilia wakati wa kuyatamka.