عن أبي مسعود الأنصاري رضي الله عنه قال:
جَاءَ رَجُلٌ إِلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَ: إِنِّي أُبْدِعَ بِي فَاحْمِلْنِي، فَقَالَ: «مَا عِنْدِي»، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَنَا أَدُلُّهُ عَلَى مَنْ يَحْمِلُهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «مَنْ دَلَّ عَلَى خَيْرٍ فَلَهُ مِثْلُ أَجْرِ فَاعِلِهِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1893]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Masoud Al-Answari -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika kipandwa changu kimeangamia nakuomba msaada wa usafiri, akasema: "Sina uwezo" Mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuonyesha kwa mtu atakayeweza kumbeba, akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Atakayeelekeza katika jambo la kheri basi atapata malipo mfano wa malipo ya mfanyaji wake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1893]
Alikuja mtu mmoja kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akasema: Hakika mimi kimeangamia kipandwa changu, nipe msaada, na unipe kipandwa kitakachonifikisha, Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akampa udhuru yakuwa yeye hana kitu cha kumsaidia, mtu mmoja akasema na alikuwepo katika mazungumzo: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi nitamuelekeza kwa mtu atakaye mbeba, akaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa yeye atashiriki katika kupata malipo na mtoaji, kwa sababu amemuelekeza muhitaji kwake.