+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«مَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيَقُلْ خَيْرًا أَوْ لِيَصْمُتْ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيُكْرِمْ جَارَهُ، وَمَنْ كَانَ يُؤْمِنُ بِاللهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ فَلْيُكْرِمْ ضَيْفَهُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 47]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na aseme la kheri au anyamaze, na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu jirani yake, na mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho basi na amkirimu mgeni wake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 47]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mja mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ambayo ndani yake kuna marejeo yake na malipo ya matendo yake, basi imani yake inamuhimiza kufanya mambo haya.
La kwanza: Kauli njema: Kama tasbihi (kusema: Sub-haanallah) na tahlili (Laa ilaaha illa llaah) na kuamrisha mema, na kukataza mabaya, na kuwasuluhisha watu, ikiwa hatofanya hivyo basi ashikamane na ukimya, na ajizuie na maudhi yake, na ahifadhi ulimi wake.
La pili: Kumkirimu jirani: Kwa kumtendea wema na kutomuudhi.
La tatu: Kumkirimu mgeni anayekuja kukutembelea: Kwa maneno mazuri na kumlisha chakula na mfano wa hayo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Imani ya Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ndio msingi wa kila kheri, na ni msukumo wa kufanya kheri.
  2. Tahadhari dhidi ya maafa ya ulimi.
  3. Dini ya Uislamu ni dini ya ukaribu na ukarimu.
  4. Mambo haya ni katika vipengele vya imani na ni katika adabu njema.
  5. Maneno mengi yanayeweza kumvuta mtu katika machukizo au uharamu, na kusalimika na hilo ni kutozungumza ila katika kheri.