+ -

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال:
«أَتَدْرُونَ مَا الْغِيبَةُ؟»، قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «ذِكْرُكَ أَخَاكَ بِمَا يَكْرَهُ»، قِيلَ: أَفَرَأَيْتَ إِنْ كَانَ فِي أَخِي مَا أَقُولُ؟ قَالَ: «إِنْ كَانَ فِيهِ مَا تَقُولُ فَقَدِ اغْتَبْتَهُ، وَإِنْ لَمْ يَكُنْ فِيهِ فَقَدْ بَهَتَّهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2589]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake-yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hivi mnajua ni nini kusengenya?", Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndio wajuzi, akasema: "Ni kumsema ndugu yako kwa yale anayoyachukia", Pakasemwa: Waonaje ikiwa niyasemayo yako kwa ndugu yangu? Akasema: "Yakiwa kwake uyasemayo utakuwa umemsengenya, na ikiwa hana basi utakuwa umemzulia uongo".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2589]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- ukweli kuhusu kusengenya kuliko haramishwa, nako ni: Kumsema muislamu asiyekuwepo kwa yale anayoyachukia, sawa sawa iwe ni katika sifa zake za kimaumbile au za kitabia, mfano: Chongo, mpiga ghushi, muongo, na mfano wa hayo katika sifa mbaya, hata kama sifa hizo anazo.
Ama zisipokuwa kwake sifa hizo hii ndio mbaya zaidi kuliko kusengenya, nako ni kuzua uongo, yaani: kumzulia mtu asiyokuwa nayo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kiasi kwamba hutoa mafundisho kwa njia ya swali.
  2. Uzuri wa adabu ya Masahaba wakiwa pamoja na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, waliposema: Mwenyezi Mungu na Mtume ndio wajuzi.
  3. Kauli ya muulizwaji kwa lile asilolijua: Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.
  4. Sheria imelinda jamii, na imehifadhi haki na udugu baina yao.
  5. Kusengenya ni haramu isipokuwa katika baadhi ya hali kwa ajili ya masilahi; Na miongoni mwake: Ni kuzuia dhulma, kiasi kwamba atamtaja aliyedhulumiwa yule aliyemdhulumu kwa yule anayeweza kumchukulia haki yake, akasema: Fulani kanidhulumu, au kanifanyia jambo hili na lile, ikiwemo pia kutaka ushauri katika swala la kuoa au ushirika au ukaribu, na mfamo wake.