عن عمران بن حصين رضي الله عنه قال: كَانَتْ بِي بَوَاسِيرُ، فَسَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَنِ الصَّلَاةِ، فَقَالَ:
«صَلِّ قَائِمًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَقَاعِدًا، فَإِنْ لَمْ تَسْتَطِعْ فَعَلَى جَنْبٍ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 1117]
المزيــد ...
Kutoka kwa Imran bin Huswain -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Niliugua bawasiri, nikamuuliza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu kusali, akasema:
"Swali ukiwa umesimama, usipoweza basi swali ukiwa umekaa, usipoweza basi ukiwa umelala ubavu".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 1117]
Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa asili katika swala ni kusali kwa kusimama, isipokuwa katika hali ya kutoweza hapo mtu atasali kwa kukaa, na ikiwa hatoweza kukaa atasali kwa ubavu.