عن عائشة رضي الله عنها أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «إن الرفق لا يكون في شيء إلا زانه، ولا ينزع من شيء إلا شانه».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Hakika upole hauwi katika kitu ispokuwa utakipendezesha, na wala hauondolewi katika kitu ispokuwa utakiharibu".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Mpole hupata mahitajio yake au baadhi yake, ama mwenye ukali hawezi kuyapata, na hata akiyapata basi ni kwa tabu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Umuhimu wa kujipamba na upole, kwani unampendezesha mtu na unamfanya mzuri katika macho ya watu na kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Kujiweka mbali na ukorofi na ukali na ugumu, kwasababu haya yanamfanya kuwa mbaya mfanyaji wake mbele za watu na kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.