عَنْ جَرِيرٍ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ يُحْرَمِ الرِّفْقَ يُحْرَمِ الْخَيْرَ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2592]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Othman -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Mwenye kunyimwa upole basi kanyimwa kheri yote"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2592]
Anatueleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwenye kunyimwa upole akawa hakuafikishwa katika mambo ya dini na dunia, na katika mambo yake mwenyewe, na yale anayoyafanya na wengine, basi atakuwa kanyimwa kheri yote.