+ -

عَنْ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رضي الله عنه:
أَنَّ رَسُولَ صَلَّى عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَخَذَ بِيَدِهِ، وَقَالَ: «يَا مُعَاذُ، وَاللَّهِ إِنِّي لَأُحِبُّكَ»، فَقَالَ: «أُوصِيكَ يَا مُعَاذُ لَا تَدَعَنَّ فِي دُبُرِ كُلِّ صَلَاةٍ تَقُولُ: اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَى ذِكْرِكَ وَشُكْرِكَ وَحُسْنِ عِبَادَتِكَ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والنسائي وأحمد] - [سنن أبي داود: 1522]
المزيــد ...

Kutoka kwa Muadhi bin Jabali -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alimshika mkono wake, na akasema: "Ewe Muadhi, Wallahi hakika mimi ninakupenda", Akasema: "Ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha mwisho wa kila swala kusema: Allaahumma ainni alaa dhikrika washukrika wahusni ibaadatika" Ewe Mwenyezi Mungu nisadie katika kukutaja na kukushukuru na kuzifanya vizuri ibada zako".

[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 1522]

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake alishika mkono wa Muadhi radhi za Allah ziwe juu yake, na akasema kumwambia: Wallahi hakika mimi ninakupenda, na ninakuusia ewe Muadhi usijekuacha kusema mwisho wa kila swala: Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie kukutaja, katika kila kauli na kitendo kinachoniweka karibu na utiifu, "na kukushukuru" kwa kutimia neema na kuzuia mabaya, "na kuzifanya vizuri ibada zako" kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kwa kumfuata Mtume rehema na amani ziwe juu yake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الرومانية Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kumueleza mtu kuwa unampenda kwa ajili ya Mwenyezi Mungu.
  2. Inapendeza kuomba dua hii mwisho wa kila swala ya faradhi na ya sunna.
  3. Katika kuomba kwa matamshi haya machache kuna mahitaji yote ya Dunia na Akhera
  4. Katika faida za kupendana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kuusiana katika na kupeana nasaha katika mambo mema na uchamungu.
  5. Amesema Attwayibi: Kumtaja Mwenyezi Mungu ni utangulizi wa kukunjua kifua, na kumshukuru ni njia ya kuzilinda neema, na kuzifanya vizuri ibada ni kujiweka mbali na yote yanayomshughulisha mtu na Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Ziada