+ -

عَنْ ‌أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ:
كَانَ أَهْلُ الْكِتَابِ يَقْرَؤُونَ التَّوْرَاةَ بِالْعِبْرَانِيَّةِ، وَيُفَسِّرُونَهَا بِالْعَرَبِيَّةِ لِأَهْلِ الْإِسْلَامِ، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا تُصَدِّقُوا أَهْلَ الْكِتَابِ وَلَا تُكَذِّبُوهُمْ، وَقُولُوا: {آمَنَّا بِاللهِ وَمَا أُنْزِلَ إِلَيْنَا} [البقرة: 136] الْآيَةَ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 4485]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Walikuwa Mayahudi na Manaswara wakiisoma Taurati kwa lugha ya Kiebrania, na kutafsiria Waislamu kwa lugha ya Kiarabu, basi akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli wala ni waongo, na semeni hivi {Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yote yaliyoteremshwa kwetu sisi} (Al-Baqara:36).

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 4485]

Ufafanuzi

Aliutahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Umma wake kutodanganyika kwa habari wanazozipokea Mayahudi na Manaswara kutoka kwenye vitabu vyao, Pindi walipokuwa Mayahudi katika zama za Mtume-Rehema na amani ziwe juu yake- wakisoma Taurati kwa lugha ya Kiebrania, nayo ni lugha ya Mayahudi, na wakitafsiri kwa lugha ya Kiarabu, Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Msiwafanye Mayahudi na Manaswara kuwa ni wakweli na wala msiwafanye kuwa ni waongo, na hivi ni kwa yale mambo ambayo hayajulikani ukweli wake wala uongo wake; Na kufanya hivyo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ametuamrisha tuamini vilivyoteremshwa kwetu katika Qur'ani, na vilivyoteremshwa kwao katika kitabu, isipokuwa hatuna namna ya kujua usahihi uliokuwepo katika vitabu hivyo ili kuepukana na visivyokuwa sahihi, kwa kuwa haikupokelewa katika sheria zetu chenye kuweka wazi ukweli wake ulioepukana na uongo wake, Hivyo tunasimama, hatuwafanyi kuwa ni wa kweli tusijekuwa pamoja nao katika zile sheria walizozibadilisha kutoka katika kitabu hicho wala hatuwafanyi kuwa ni waongo; huenda likawa jambo ni sahihi, hivyo tukawa ni wenye kupinga kile alichotuamrisha tukiamini, Na ametuamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- tuseme: {Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale yote aliyoyateremsha kwetu sisi, na yaliyoteremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-haqa na As-baatwi, na aliyopewa Mussa na Issa na waliyopewa Manabii kutoka kwa Mola wao, hatutofautishi yeyote miongoni mwao na sisi kwake yeye tumejisalimisha} (Al-Baqara:136).

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Waliyoyaeleza Mayahudi na Manaswara, yapo katika sehemu tatu:
  2. Sehemu ya kwanza inakwenda sawa na Qur'ani na Sunna hivyo sehemu hii inakubaliwa. Sehemu ya pili: Inatofautiana na Qur'ani na Sunna, sehemu hii ni batili hufanywa kuwa ni ya uongo. Sehemu ya tatu: Hakuna kwenye Qur'ani wala Sunna habari inayohusu ukweli wake au uongo wake, basi habari kama hii haifanywi kuwa ya kweli au ya uongo.