عن أنس رضي الله عنه قال: قال النبي صلى الله عليه وسلم:
«لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَالِدِهِ وَوَلَدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 15]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hawezi kua na imani mmoja wenu mpaka nipendeke kwake kuliko wazazi wake na mwanaye na watu wote".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 15]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa muislamu hawezi kua na imani kamili mpaka atangulize mapenzi ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuliko mapenzi ya mama yake na baba yake na kijana wake wa kuime na wa kike na watu wote, na mapenzi yanaambatana na kumtii na kumtetea, na kuacha kumuasi.