+ -

عَن عَبْدِ اللَّهِ بنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَ:
«مَنِ اسْتَطَاعَ البَاءَةَ فَلْيَتَزَوَّجْ، فَإِنَّهُ أَغَضُّ لِلْبَصَرِ، وَأَحْصَنُ لِلْفَرْجِ، وَمَنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَعَلَيْهِ بِالصَّوْمِ، فَإِنَّهُ لَهُ وِجَاءٌ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1905]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Masudi radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Siku moja tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema:
"Enyi kongamano la vijana mwenye uwezo miongoni mwenu wa kuoa na aoe, kwani ndoa ni sababu ya kuinamisha macho na kulinda tupu, na asiekuwa na uwezo basi ajilazimishe kufunga, hakika funga kwake itakata matamanio".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1905]

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake amewahimiza wenye uwezo wa tendo la ndoa na gharama ya ndoa waoe; kwani hilo Iinahifadhi macho yake kutokana na mambo yaliyokatazwa, linalinda usafi wake wa mwili, na linamzuia asiingie katika uasherati, ambaye hawezi kukidhi mahitaji ya ndoa hali ya kuwa ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa basi ni lazima afunge, kwani hii itakata matamanio ya tupu na shari ya manii.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الصربية الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uislamu umechunga sana sababu za mtu kujizuia na machafu na kusalimika na machafu.
  2. Himizo la kufunga swaum kwa ambaye hatoweza gharama za ndoa; kwa sababu hudhoofisha matamanio.
  3. Kufunga kunafananishwa na kuhasiwa; Kwa sababu kuhasi ni kuchubua mishipa ya korodani mbili, na kwa kitendo hicho hupotea matamani ya tendo la ndoa, hivyo hivyo swaumu hudhoofisha hamu ya tendo la ndoa.