عَنْ عُثْمَانَ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«مَا مِنَ امْرِئٍ مُسْلِمٍ تَحْضُرُهُ صَلَاةٌ مَكْتُوبَةٌ فَيُحْسِنُ وُضُوءَهَا وَخُشُوعَهَا وَرُكُوعَهَا، إِلَّا كَانَتْ كَفَّارَةً لِمَا قَبْلَهَا مِنَ الذُّنُوبِ، مَا لَمْ يُؤْتِ كَبِيرَةً، وَذَلِكَ الدَّهْرَ كُلَّهُ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 228]
المزيــد ...
kutoka kwa Othmani Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani za Allah ziwe juu yake akisema:
"Hakuna Muislamu yeyote atafikiwa na Sala ya lazima kisha akaufanya vizuri udhu wake, na Unyenyekevu wake na Rakaa zake, isipokuwa inakuwa ni kifuta madhambi yaliyo kuwa kabla ya Sala, kwa muda ambao hajafanya madhambi makubwa, na hivyo ndivyo ilivyo kila siku".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 228]
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa hakuna muislamu atakayekutwa na wakati wa swala ya faradhi akatawadha vizuri udhu wake na ukaukamilisha, kisha akawa na unyenyekevu ndani ya swala yake kiasi kwamba ukawa moyo wake na viungo vyake vyote vimeelekea kwa Mwenyezi Mungu akivuta picha ya utukufu wake, na akatimiza vitendo vya swala kama rukuu na sijida na vinginevyo, isipokuwa swala hii itakuwa ni kifutio cha madhambi madogo madogo yaliyokuwa kabla yake, madam hajafanya dhambi katika madhambi makubwa, na fadhila hii ni endelevu kwa muda wote na katika kila swala.