عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِيَّاكُمْ وَالدُّخُولَ عَلَى النِّسَاءِ» فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ الأَنْصَارِ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَفَرَأَيْتَ الحَمْوَ؟ قَالَ: «الحَمْوُ المَوْتُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5232]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Uqbah bin Aamir -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake:
"Tahadharini sana na kuingia/kukaa kwa wanawake" Mtu mmoja katika Maanswari akasema: Ewe Mtume wa Allah vipi kuhusu shemeji? Akasema: "Shemeji ni kifo".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5232]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake swala la kuchanganyikana na wanawake wa kando, na akasema: Jiepusheni sana kuingia kwa wanawake, na wanawake watahadhari kuingia kwa wanaume.
Akasema mtu mmoja miongoni mwa Manswari (watu wa Madina): Wasemaje kuhusu ndugu wa karibu wa mume; kama kaka wa mume na mtoto wa kaka yake, na ami yake na mtoto wa ami yake, na kijana wa dada yake, na mfano wa hao katika wale wa halali kwao kumuoa akiwa hajaolewa?
Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Mtahadharini kama mnavyokitahadhari kifo! Kwa sababu kukaa faragha na mashemeji kunapelekea fitina na maangamivu katika dini, ndugu wa mume wasiokuwa baba zake na wanawe, hawa wanatakiwa zaidi kuzuiliwa kuliko hata mtu wa kando; kwa sababu kukaa faragha na ndugu wa mume ni zaidi ya kukaa faragha na mtu mwingine, na shari iko karibu zaidi kwake kutokea kuliko hata kwa asiyekuwa yeye, na kuna uwezekano mkubwa wa kutokea; kwa sababu anauwezekano mkubwa wa kumfikia mwanamke na kukaa naye faragha pasina mtu wa kuwakemea, na ni kwa sababu hana budi lazima aonane naye kwakuwa ni ndugu wa mume, na ni vigumu kumzuia, kwa sababu tamaduni za watu zimezoeleka kulipuuza hilo, mtu akakaa faragha na mke wa kaka yake; hivyo anafanana na kifo katika ubaya na madhara, tofauti na mwanaume wa kando kwani huyo watu humtahadhari.