عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «لا نِكاح إلا بِوَلِيّ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه والدارمي وأحمد]
المزيــد ...
kutoka kwa Abii Musa Al-Ash'ariy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, amesema: "Hakuna ndoa bila walii (msimamizi)".
Sahihi - Imepokelewa na Ibnu Maajah
Imeonyesha hadithi juu ya kumzingatia walii katika kufunga ndoa nakuwa hilo ni sharti la kusihi kwake, hivyo haikubaliki ndoa ila kwa walii, anayesimamia ufungishaji wa ndoa, na ni sharti kwa walii: Utuuzima (kubalehe), na kuwa mwanaume, na uelevu katika kujua maslahi ya ndoa, na kuwiana katika dini (kuwa katika dini moja) kati ya msimamizi na msimamiwa, ambaye hatosifika kwa sifa hizi, basi atakuwa hastahiki kusimamia kufungisha ndoa, ikishindikana basi msimamizi wake atakuwa kiongozi.