«إِنَّ اللهَ يُحِبُّ الْعَبْدَ التَّقِيَّ الْغَنِيَّ الْخَفِيَّ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2965]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Sa'd bin Abii Waqas -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakika Mwenyezi Mungu humpenda mja mchamungu, mwenye kutosheka, mnyenyekevu".
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anawapenda baadhi ya waja wake,
Na miongoni mwao ni mchamungu: Mwenye kutekeleza amri za Allah, mwenye kuyaepuka makatazo yake.
Na anampenda mwenye kutosheka: Aliyetosheka kutowahitajia watu kwa kumuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hageuki kwa mwingine.
Na anampenda mnyenyekevu: Mwenye kujinyenyekeza, mwenye kumuabudu Mola wake Mlezi, mwenye kujishughulisha na yenye kumnufaisha, ambaye hashughuliki na kutaka yeyote amjue au amzungumze kwa sifa au shukurani.
إثبات صفة المحبة لله –وهي على الوجه اللائق به-، وأنه يحب العبد الطائع.المراجع تحتاج تصحيح