عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ الْعَاصِ رضي الله عنهما أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يَدْعُو بِهَؤُلَاءِ الْكَلِمَاتِ:
«اللَّهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ غَلَبَةِ الدَّيْنِ، وَغَلَبَةِ الْعَدُوِّ، وَشَمَاتَةِ الْأَعْدَاءِ».
[صحيح] - [رواه النسائي وأحمد] - [سنن النسائي: 5475]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdillah bin Amry bin Aaswi radhi za Allah ziwe juu yao wote wawili yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiomba kwa maneno haya:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui"
[Sahihi] - - [سنن النسائي - 5475]
Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na mambo haya:
La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda" na ninajikabidhi na kujiweka "kwako" si kwa mwingine, "kutokana na kuelemewa na deni" na kunitenza nguvu na misukosuko yake, na ninakuomba msaada wa kulilipa na kulitimiza.
La pili: "Na kuzidiwa na adui" na kunitenza nguvu na kunitawala kimabavu, na ninakuomba uzuie adha zake, na unipe ushindi juu yake.
La tatu: "Na kutukanwa na maadui" na kufurahi kwao kwa yale yanayowafika waislamu miongoni mwa mabalaa na misiba.