+ -

عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه قَالَ:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُكْثِرُ أَنْ يَقُولَ: «يَا مُقَلِّبَ القُلُوبِ ثَبِّتْ قَلْبِي عَلَى دِينِكَ»، فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللهِ، آمَنَّا بِكَ وَبِمَا جِئْتَ بِهِ فَهَلْ تَخَافُ عَلَيْنَا؟ قَالَ: «نَعَمْ، إِنَّ القُلُوبَ بَيْنَ أُصْبُعَيْنِ مِنْ أَصَابِعِ اللهِ يُقَلِّبُهَا كَيْفَ يَشَاءُ».

[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 2140]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.” Basi nikasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, tunakuamini wewe na ulicholeta, je unatuhofia? Akasema: "Ndio, nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, anazigeuza kwa namna atakavyo"

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2140]

Ufafanuzi

Dua nyingi za Mtume rehema na amani ziwe juu yake zilikuwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu uthabiti katika dini na utiifu, na kujiepusha na kupinda na upotofu. Anas bin Malik radhi za Allah ziwe juu yake alistaajabu kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akiiomba dua hii mara kwa mara, basi Mtume rehema na amani zimshukie akamwambia kuwa nyoyo ziko baina ya vidole viwili vya Mwenyezi Mungu, huzigeuza apendavyo, hivyo, moyo ni kituo cha imani na ukafiri, na moyo umeitwa Qalbu kwa sababu ya kugeukageuka kwake mara kwa mara, moyo hugeuka sana kuliko chungu kinapokusanyika kile kinachotokota ndani yake. Amtakaye Mwenyezi Mungu huudumisha moyo wake katika uongofu na uthabiti katika Dini, na anayemtaka Mwenyezi Mungu huugeuza moyo wake kutoka katika uongofu na kuupeleka katika upotofu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الصربية الرومانية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kujisalimisha kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Mola wake Mlezi na kunyenyekea kwake, na kuuelekeza umma kuliomba hilo.
  2. Umuhimu wa kuwa na msimamo na uthabiti katika dini, na kuwa kinachozingatiwa ni hatima ya mtu ya maisha yake.
  3. Mja hawezi kujitosheleza mwenyewe hata kwa kupepesa jicho bila ya kutiwa uthabiti na Mwenyezi Mungu katika Uislamu.
  4. Himizo la kuomba dua hii kwa wingi, kwa kumuiga Mtume rehema na amani ziwe juu yake.
  5. Kudumu katika Uislamu ni neema kubwa ambayo mja anatakiwa kuifanyia juhudi na kumshukuru Mola wake Mlezi.