+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَمَّا خَلَقَ اللَّهُ الْجَنَّةَ وَالنَّارَ أَرْسَلَ جِبْرِيلَ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِلَى الْجَنَّةِ، فَقَالَ: انْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا. فَنَظَرَ إِلَيْهَا فَرَجَعَ، فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا. فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ، فَقَالَ: اذْهَبْ إِلَيْهَا فَانْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا. فَنَظَرَ إِلَيْهَا، فَإِذَا هِيَ قَدْ حُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ، فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ لَا يَدْخُلَهَا أَحَدٌ. قَالَ: اذْهَبْ فَانْظُرْ إِلَى النَّارِ وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا. فَنَظَرَ إِلَيْهَا فَإِذَا هِيَ يَرْكَبُ بَعْضُهَا بَعْضًا، فَرَجَعَ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَا يَدْخُلُهَا أَحَدٌ. فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالشَّهَوَاتِ، فَقَالَ: ارْجِعْ فَانْظُرْ إِلَيْهَا. فَنَظَرَ إِلَيْهَا فَإِذَا هِيَ قَدْ حُفَّتْ بِالشَّهَوَاتِ، فَرَجَعَ وَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ لَا يَنْجُوَ مِنْهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا».

[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي] - [سنن أبي داود: 4744]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira -Allah amridhie- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto alimtuma Malaika Jibril -Amani iwe juu yake- aende peponi Akamwambia: Iangalie hiyo pepo na yale niliyo waandalia humo watu wa peponi, basi Jibrili akaiangalia Pepo kisha akarudi, akasema: Naapa kwa utukufu Wako ewe Mwenyezi Mungu hatozisikia mtu yeyote habari za pepo kisha asiingie humo, kisha akamuamrisha kuizungushia Pepo hiyo mambo yenye kuchukiza, kisha akamwambia nenda tena ukaiangalie na uangalie yale niyowaandalia watu wake humo peponi. Basi akaiangalia ghafla akaiona imezungushwa vyenye kuchukiza, akasema: Naapa kwa utukufu Wako kwa hakika ninahofia kuwa hatoingia mtu yeyote. Akasema kumwambia Jibrili nenda na uuangalie Moto na yale niliyo waandalia humo watu wa Motoni. Basi akauangalia Moto na akauona Moto ulivyopambwa, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu Wako hatoingia yeyote humo, basi akaamrisha ukazungushwa mambo yenye kutamanisha, basi akamwambia: Rudi na uuangalie tena. Basi akauangalia akaukuta umepambwa na kuzungushwa yenye kutamanisha, basi akarudi na akasema: Naapa kwa utukufu wako kwa hakika nahofia yakuwa hatosalimika mtu yeyote isipokuwa ataingia Motoni."

[Ni nzuri] - - [سنن أبي داود - 4744]

Ufafanuzi

Alitoa habari Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa Mwenyezi Mungu alipoumba Pepo na Moto, alimwambia Jibril -Amani iwe juu yake- nenda mpaka Peponi na uangalie humo, basi akaenda na akaangalia ndani ya Pepo kisha akarudi, Basi Jibrili akasema: Ewe Mola wangu, nina apa kwa utukufu wako kuwa hatosikia yeyote habari za Pepo na yaliyo humo miongoni mwa neema na mazuri na kheri mbalimbali isipokuwa atapenda kuingia humo, na atafanya matendo ili aweze kuingia humo, Kisha Mwenyezi Mungu baada ya kauli hiyo akaizungushia pepo mambo yenye kuchukiza na magumu, yakiwemo kutekeleza maamrisho na kujiepusha na makatazo, basi ikawa mwenye kutaka kuingia humo anatakiwa akivuke kizingiti cha hayo yenye kuchukiza. Kisha Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: "Ewe Jibril nenda na utazame Pepo", Baada ya kuwa amekwisha izungusha mambo yenye kuchukiza, Basi akaenda kisha akaitazama, kisha akaja na akasema: Nina apa kwa utukufu wako ninahofia kuwa hatoingia yeyote kwa sababu ya mambo mazito na magumu ambayo yapo kwenye njia ya kuweza kuingia katika Pepo. Na Mwenyezi Mungu alipoumba Moto, alisema: Ewe Jibril! nenda nauutazame Moto, basi akaenda na akautazama, Kisha Jibril akaja na akasema; Ewe Mola wangu, nina apa kwa utukufu wako, kuwa hatosikia yeyote habari ya vilivyomo humo miongoni mwa adhabu na matatizo mateso isipokuwa atachukia ili asiingie humo na atajiweka mbali na vitakavyomsababishia kuingia humo. Kisha Mwenyezi Mungu akauzungushia Moto na akaweka njia ya kuufikia Moto huo ni vitu vyenye kutamanisha na vyenye ladha, kisha akasema: Ewe Jibril, nenda na uutazame Moto, Basi Jibril akaenda na akautazama moto, kisha akaja na akasema: Ewe Mola wangu naapa kwa utukufu wako kwa hakika nimepatwa na hofu na uoga na nimepatwa na huruma yakuwa hatosalimika yeyote na moto huo kwa namna ulivyozungukwa moto na vyenye kutamanisha na vyenye ladha.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف البلغارية Luqadda Asariga اليونانية الأوزبكية الأوكرانية الجورجية اللينجالا المقدونية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuamini kuwa Pepo na Moto kwa sasa vyote hivyo vipo.
  2. Ulazima wa kuamini mambo ya ghaibu (yasiyo onekana), na kuamini kila kilichokuja kutoka kwa, Mwenyezi Mungu na Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  3. Umuhimu wa kusubiri kwenye mambo yenye kuudhi kwa sababu hiyo ni njia ya kumfikisha mtu peponi.
  4. Umuhimu wa kujiepusha na mambo yaliyoharamishwa; kwa sababu hiyo ni njia ya kumfikisha mtu Motoni.
  5. Pepo imezungushwa yenye kuchukiza, na Moto umezungushwa yenye kutamanisha, nayo hupelekea kuingia kwenye majaribu katika maisha haya ya Duniani.
  6. Njia ya kwenda Peponi ni ngumu na ina tabu nyingi, na inahitajia subira kuvumilia mateso pamoja na kuwa na imani, na njia ya kwenda Motoni imejaa vyenye kuvutia na kutamanisha hapa duniani.