+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«أَرَأَيْتُمْ لَوْ أَنَّ نَهَرًا بِبَابِ أَحَدِكُمْ يَغْتَسِلُ فِيهِ كُلَّ يَوْمٍ خَمْسًا، مَا تَقُولُ ذَلِكَ يُبْقِي مِنْ دَرَنِهِ؟» قَالُوا: لَا يُبْقِي مِنْ دَرَنِهِ شَيْئًا، قَالَ: «فَذَلِكَ مِثْلُ الصَّلَوَاتِ الخَمْسِ، يَمْحُو اللَّهُ بِهِ الخَطَايَا».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 528]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hebu nielezeni lau kama Mto ungelikua mlangoni kwa mmoja wenu akioga humo kila siku mara tano, unasemaje kuhusu hilo, kunaweza kubaki na uchafu katika mwili wake?" Wakasema: Hautobakiza uchafu wowote, akasema: " Huu ndio mfano wa swala tano, Mwenyezi Mungu hufuta makosa kwa swala hizo".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 528]

Ufafanuzi

Amefananisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- swala tano za kila usiku na mchana katika kuondoa kwake na kufuta kwake madhambi madogo ni sawa na Mto ulioko mlangoni kwa mtu akioga humo kila siku mara tano, hautobakiza chochote katika uchafu wake.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila hizi ni maalum kwa kufuta madhambi madogo, ama makubwa hayo ni lazima kuwe na toba.
  2. Fadhila za kutekeleza swala tano na kuzihifadhi kwa sharti zake na nguzo zake na wajibu wake na sunna zake.