عن تميم الداري رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«الدِّينُ النَّصِيحَةُ» قُلْنَا: لِمَنْ؟ قَالَ: «لِلهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِأَئِمَّةِ الْمُسْلِمِينَ وَعَامَّتِهِمْ».

Imepokewa Kutoka kwa Tamim Ad-dari -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Yakuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Amesema:
"Dini ni nasaha" Tukasema: Kwa ajili ya nani? Akasema: "Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na kitabu chake, na Mtume wake, na kwa viongozi wa waislamu na watu wote."

Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim Swahiih Muslim - 55

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa dini imesimama katika misingi ya kutakasa nia (Ikhlas) na ukweli, ili itekelezwe kama alivyowajibisha Mwenyezi Mungu, kikamilifu bila uzembe au udanganyifu.
Akaulizwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Nasaha huwa kwa ajili ya nani? Akasema:
Kwanza: Nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: Kwa kutakasa matendo kwa ajili yake, na kutomshirikisha mwingine pamoja naye, na tuamini ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, na kuzitukuza amri zake, na kulingania watu katika kumuamini.
Pili: Nasaha ni kwa ajili ya kitabu cha Mwenyezi Mungu nacho ni Qur'ani Tukufu: Tuitakidi kuwa ni maneno yake, na ni kitabu chake cha mwisho, nakuwa kimefuta sheria zote zilizokuwa kabla yake, na tunakitukuza, na tunakisoma ukweli wa kukisoma, na tunazifanyia kazi aya zake za wazi, na tunazikubali zenye kutatiza, na tunapinga upotoshaji wa wenye kupindisha, na tunayazingatia mawaidha yake, na kuieneza elimu yake, na kuwalingania watu kwayo.
Tatu: Nasaha kwa ajili ya Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake-: Tuitakidi kuwa yeye ni Mtume wa mwisho, na tumsadikishe katika yale aliyokuja nayo, na tutekeleze amri zake, na tuyaepuke makatazo yake, na tusimuabudu Allah isipokuwa kwa yale aliyokuja nayo, na tuitukuze haki yake, na tumuheshimu, na tuutangaze ujumbe wake, na tuisambaze sheria yake, na tuzikanushe tuhuma dhidi yake.
Nne: Nasaha kwa viongozi wa waislamu: Kwa kuwasaidia katika haki, na kutozozana nao katika uongozi, na kuwasikiliza na kuwatii katika mambo ya kumtii Mwenyezi Mungu.
Tano: Nasaha kwa waislamu: Kwa kuwafanyia wema na kuwalingania, na kuzuia maudhi dhidi yao, na kuwapendelea kheri, na kusaidizana nao katika wema na uchamungu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Amri ya kunasihiana ni kwa watu wote.
  2. Ukubwa na utukufu wa nafasi ya nasaha katika dini.
  3. Dini imekusanya mambo ya itikadi, maneno, na matendo.
  4. Miongoni mwa nasaha ni kujinasihi mwenyewe kutomfanyia udanganyifu yule mwenye kunasihiwa pamoja na kumtakia kheri.
  5. Uzuri wa mafundisho ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, kiasi kwamba anataja jambo kwa ujumla kisha analifafanua.
  6. Kuanza na lenye umuhimu zaidi kisha linalofuata, kwani alianza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kwa nasaha kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha kitabu chake, kisha Mtume wake -Rehema na amani ziwe juu yake- kisha viongozi wa waislamu, kisha watu wote kwa ujumla.

Kuonyesha Tafsiri

69 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
JA 日本語 اليابانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
FF Fulfulde الفولانية
IT Italiano الإيطالية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
BG Български البلغارية
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
EL Ελληνικά اليونانية
AK Akan الأكانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
LN Lingala اللينجالا
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
BM Bambara البامبارية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
DA Dansk الدنماركية
RN Kirundi الكيروندي
KMR Kurmancî الكرمنجية
MS Bahasa Melayu الملايو