عَنْ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«الرَّضَاعَةُ تُحَرِّمُ مَا تُحَرِّمُ الوِلَادَةُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [الأربعون النووية: 44]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Kunyonya pamoja kuna haramisha yale yanayo haramishwa na kuzaliwa pamoja."
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [الأربعون النووية - 44]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa inakuwa haramu kwa kunyonya sawa na uharamu wa kuzaliwa na wa nasaba kama mjomba au baba mdogo au kaka n.k. na kunyonya kuna halalisha yale yanayohalalishwa na kuzaliwa miongoni mwa hukumu.