عن أبي هريرة رضي الله عنه قال:
لَعَنَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الرَّاشِيَ وَالْمُرْتَشِيَ فِي الْحُكْمِ.
[صحيح] - [رواه الترمذي وأحمد] - [سنن الترمذي: 1336]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
"Amemlaani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Rehema na Amani ziwe juu yake- mtoa rushwa na mpokea rushwa katika hukumu".
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 1336]
Aliomba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu mtoa rushwa na mchukuaji wake na mpokeaji wake.
Na miongoni mwake ni kile kinachotolewa kwa mahakimu ili wapindishe hukumu wanayoisimamia; ili mtoaji aitumie kama njia ya kufikia lengo lake pasina haki.