عَنْ أَبِي بَكْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«لَنْ يُفْلِحَ قَوْمٌ وَلَّوْا أَمْرَهُمُ امْرَأَةً».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 4425]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Bakra -radhi za Allah ziwe juu yake- yakuwa yeye alimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hawatofanikiwa watu waliomkabidhi utawala wao mwanamke".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 4425]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba hawatofanikiwa watu kwa kupata wanayoyataka pindi watakapomtawalisha na kummilikisha mwanamke swala la hukumu au usimamizi wa dola au wizara.