عن أبي هُريرة رضي الله عنه مرفوعًا: «إذا قلتَ لصاحبك: أَنْصِتْ يوم الجمعة والإمام يَخْطُبُ، فقد لَغَوْتَ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie- Hadithi Marfu'u: "Utakaposema kumwambia mwenzio: Nyamaza siku ya ijumaa na Imamu ana hutubu, utakuwa umefanya mchezo.
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Na katika alama kubwa za Ijumaa ni hotuba mbili, na katika malengo yake ni kuwakumbusha watu na kuwaelekeza, na katika Adabu za lazima kwa msikilizaji: ni kunyamaza ndani ya hotuba hizo mbili na kumsikiliza hatibu, ili azingatie mawaidha, na ndiyo maana alitahadharisha Mtume rehema na Amani zimfikie- kutokana na kuzungumza, hata kama ni kwa kitu kidogo, mfano kumkataza mwenzie asizungumze hata kwa neno: "Nyamaza" na atakayezungumza na imamu ana hutubu atakuwa kafanya mchezo, na atakosa fadhila za Ijumaa; kwasababu atakuwa kaleta kinachomshughulisha na kumshughulisha mwingine kutosikiliza hotuba.