عن عثمان بن عفان رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«مَنْ تَوَضَّأَ فَأَحْسَنَ الْوُضُوءَ خَرَجَتْ خَطَايَاهُ مِنْ جَسَدِهِ حَتَّى تَخْرُجَ مِنْ تَحْتِ أَظْفَارِهِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 245]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Othman bi Affan -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake:
"Atakayetawadha na akaufanya vizuri udhu wake, hutoka makosa yake ndani ya mwili wake mpaka yakatiririka kutoka chini ya kucha zake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 245]
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetawadha kwa kuchunga sunna za udhu na adabu zake, hilo litakuwa katika sababu za kusamehewa makosa na kufuta madhambi, "Mpaka yatoke" madhambi yake kutoka chini ya kucha za mikono yake na miguu yake.