عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِنَّ الدِّينَ يُسْرٌ، وَلَنْ يُشَادَّ الدِّينَ أَحَدٌ إِلَّا غَلَبَهُ، فَسَدِّدُوا وَقَارِبُوا، وَأَبْشِرُوا، وَاسْتَعِينُوا بِالْغَدْوَةِ وَالرَّوْحَةِ وَشَيْءٍ مِنَ الدُّلْجَةِ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 39]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Hakika dini ni nyepesi, na hatoifanyia mkazo dini yeyote ila itamshinda, basi shikamaneni na mfanye kadiri ya uwezo yanayoweza kukuwekeni karibu, na toeni bishara, na takeni msaada nyakati za asubuhi au mchana au sehemu ya usiku"
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 39]
Alibainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Dini ya Uislamu imeegemezwa katika usahilishaji na wepesi katika mambo yake yote, na usahilishaji unathibitishwa pale panapotokea sababu ya kutokuwa na uwezo na haja, kwa sababu kuzama ndani sana katika matendo ya dini na kuacha upole matokeo yake ni kutoweza na kukoma kufanya amali zote au baadhi yake. ... Kisha akahimiza rehema na amani ziwe juu yake kuwa kati na kati pasina kupitiliza; Mja asifanye uzembe katika yale aliyoamrishwa, na wala asijibebeshe asiyoyaweza, akishindwa kuifanya amali nzima kamili; basi afanye inayokaribiana na hiyo.
Alitoa habari njema Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya malipo makubwa ya amali ya kudumu, hata ikiwa ni kidogo, kwa wale ambao hawawezi kufanya amali nzima kikamilifu, kwa sababu ikiwa kushindwa huko hakutokani na yeye mwenyewe, hakutopelekea kupunguzwa kwa malipo yake.
Na kwa kuwa ulimwengu huu kwa hakika ni mahala pa kusafiri na mapito ya kuelekea Akhera, ameamrisha rehema na amani ziwe juu yake kutaka msaada katika kudumisha ibada kwa kuiweka nyakati tatu ambazo mtu anakuwa na hamasa:
Wakati wa kwanza ni Asubuhi: Kwa kwenda mwanzo wa mchana; kati ya swala ya Alfajiri na kuchomoza jua.
Wa pili: Mchana: Kwa kwenda wakati linapopinduka jua.
Wa tatu: Giza: kwa mwendo wa usiku mzima au sehemu yake, na kwa sababu amali ya usiku ni ngumu zaidi kuliko amali ya mchana, akaamrisha kufanya baadhi yake, kwa kauli yake: Na baadhi ya usiku.