1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni

عَنْ ابْنَ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«إِذَا رَأَيْتُمُوهُ فَصُومُوا، وَإِذَا رَأَيْتُمُوهُ فَأَفْطِرُوا، فَإِنْ غُمَّ عَلَيْكُمْ فَاقْدُرُوا لَهُ».

Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- Amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mtakapouona basi fungeni, na mtakapouona basi fungueni, ukifunikwa kwenu nyinyi basi ukadirieni".

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 1900

Ufafanuzi

Alibainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuingia kwa mwezi wa Ramadhani na kutoka kwake, akasema: Mtakapouona mwandamo wa Ramadhani basi fungeni, yakikukingeni mawingu kati yake na nyie, basi hesabuni siku thelathini za mwezi Shaaban, na mkiuona mwandamo wa mwezi Shawal basi fungueni, yakikukingeni mawingu na ukafichikana kwenu; basi hesabuni siku thelathini za mwezi Ramadhani.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kinachotakiwa ni kutegemea kuona na si hesabu katika kuthibitisha kuingia kwa mwezi.
  2. Amenukuu bin Mundhiri makubaliano ya wanachuoni kuwa hakuna ulazima wa kufunga ikiwa kuingia kwa mwezi wa Ramadhani ni kwa hesabu pekee pasina kuuona.
  3. Ulazima wa kukamilisha mwezi Shaaban siku thelathini pindi mawingu au mfano wake yatakapoziba kuuona mwandamo wa mwezi Ramadhani.
  4. Mwezi unaozingatia mwandamo hauwi isipokuwa ni siku ishirini na tisa, au siku thelathini.
  5. Ulazima wa kukamilisha Ramadhani siku thelathini mawingu au mfano wake yatakapoziba kati yake na mwandamo wa Shawal.
  6. Atakayekuwa katika mazingira ambayo hakuna mtu wa kufuatilia maswala ya waislamu katika swaumu, au akawa ni katika watu wanaopoteza kumbukumbu, basi analazimika kulichunga hilo na afuatilie kwa mtu atakayemthibitishia hilo kwa kuuona au kwa mtu mwingine kuuona, atafunga na kufungua kwa taarifa hiyo.

Kuonyesha Tafsiri

51 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية