1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Mambo mazuri na Adabu- Heshima.

Hadithi Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako

عَنْ عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: كَانَ مِنْ دُعَاءِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ زَوَالِ نِعْمَتِكَ، وَتَحَوُّلِ عَافِيَتِكَ، وَفُجَاءَةِ نِقْمَتِكَ، وَجَمِيعِ سَخَطِكَ».

kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Ilikuwa miongoni mwa dua za Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- ni kusema:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako"

Sahihi Imepokelewa Imamu Muslim Swahiih Muslim - 2739

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba kinga ya mambo manne:
La kwanza: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na kuondokewa na neema zako" za dini na dunia, na nibakie madhubuti ndani ya Uislamu, na najiweka mbali kutoangukia katika maasi yanayoondosha neema.
La pili: "Na kubadilika ghafla neema zako" Kubadilika kwake na kuwa balaa; ninakuomba afya isiyo na kikomo, na kusalimika dhidi ya mabalaa na magonjwa.
La tatu: "Na kufikwa ghafla na adhabu zako" kama vile balaa au maasi, gharika na adhabu vinapokuja ghafla, huwa hakuna muda wa kutubia na kurekebisha mabaya, na hapa hufikwa na adhabu kali na kubwa mno.
La nne: "na hasira zako zote" na sababu zenye kupelekea kupata hasira zako; kwani yeyote utakayemchukia basi atakuwa kapata hasara.
Na alileta Mtume rehema na amani ziwe juu yake tamko la wingi; ili likusanye mpaka sababu za hasira zake Aliyetakasika na kutukuka miongoni mwa kauli na matendo na itikadi.

Katika Faida za Hadithi

  1. Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhitaji kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Kuomba kinga huku kumeambatana na: Taufiki ya kushukuru neema, na hifadhi ya kutotumbukia ndani ya maasi; kwa sababu huondoa neema.
  3. Pupa ya kujiweka mbali na maeneo ya hasira za Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  4. Aliomba kinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kufikwa ghafla na hasira za Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu akiamua kumlipiza mja kwa mabaya anayoyafanya basi yatamfika mabalaa asiyoweza kuyazuia, na hayazuiliwi na viumbe wengine, hata wakikusanyika wote.
  5. Alijikinga Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kutoweka kwa afya yake Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwa sababu endapo Mungu atampendelea kwa kumpa afya yake, basi atakuwa kapata bahati ya kupata kheri zote za dunia na Akhera, ikimuondokea basi atakuwa kapatwa na shari ya dunia na Akhera, kwani afya ndio sababu ya kutengemaa dini na dunia.

Kuonyesha Tafsiri

50 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية