«لَا تُطْرُونِي كَمَا أَطْرَتِ النَّصَارَى ابْنَ مَرْيَمَ؛ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدُهُ، فَقُولُوا: عَبْدُ اللهِ وَرَسُولُهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 3445]
المزيــد ...
Imepokelewa Kutoka kwa Omar bin Khattwab -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Msichupe mipaka katika kunisifu, kama walivyochupa mipaka Wakristo kwa mwana wa Mariam; Bila shaka, mimi ni mja wake, na semeni: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 3445]
Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kupitiliza na kuvuka mpaka wa kisheria katika kumsifu, na kumsifu kwa sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu na matendo yake ambayo ni yake pekee, au kusema kuwa anajua mambo yaliyo jificha, au anastahiki kuombwa pamoja na Mwenyezi Mungu, kama walivyofanya Wakristo kwa Issa mwana wa Mariam -Amani iwe juu yake- Kisha akaweka wazi kuwa yeye ni mja wa Mwenyezi Mungu, na akaamrisha tuseme kuhusu yeye: Mja wa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake.
ما حذَّر منه النبي صلى الله عليه وسلم قد وقع في هذه الأمة، فغَلَتْ طائفة بالرسول الله صلى الله عليه وسلم، وطائفة في أهل البيت، وطائفة في الأولياء، فوقعوا في الشرك.التعريف يحذف لانه مضاف اليه فغَلَتْ طائفة بالرسول الله