+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا تَوَضَّأَ أَحَدُكُمْ فَلْيَجْعَلْ فِي أَنْفِهِ ثُمَّ لِيَنْثُرْ، وَمَنِ اسْتَجْمَرَ فَلْيُوتِرْ، وَإِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلْيَغْسِلْ يَدَهُ قَبْلَ أَنْ يُدْخِلَهَا فِي وَضُوئِهِ، فَإِنَّ أَحَدَكُمْ لاَ يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدُهُ». ولفظ مسلم: «إِذَا اسْتَيْقَظَ أَحَدُكُمْ مِنْ نَوْمِهِ فَلَا يَغْمِسْ يَدَهُ فِي الْإِنَاءِ حَتَّى يَغْسِلَهَا ثَلَاثًا، فَإِنَّهُ لَا يَدْرِي أَيْنَ بَاتَتْ يَدُهُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 162]
المزيــد ...

Imepokewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakapotawadha mmoja wenu basi na aweke maji puani mwake kisha ayapenge, na atakayestanji kwa mawe basi afanye yawe witiri, na atakapo amka mmoja wenu toka usingizini basi na aoshe mikono yake kabla ya kuingiza ndani ya chombo chake, kwani mmoja wenu hajui ni wapi ulilala mkono wake". Na lafudhi ya Muslim: "Atakapoamka mmoja wenu kutoka usingizini kwake basi asizamishe mkono wake ndani ya chombo mpaka auoshe mara tatu, kwani hajui ni wapi ulilala mkono wake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 162]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- baadhi ya hukumu za twahara, miongoni mwake: Ya kwanza: Nikuwa mwenye kutawadha ni lazima aingize maji puani mwake kwa kuyavuta kwa pumzi, kisha ayatoe kwa pumzi pia. Ya pili: Nikuwa atakayetaka kusafisha udhia uliomtoka na kuuondoa pasina kutumia maji kama kwa jiwe na mfano wake, basi kusafisha kwake kuwe kwa idadi ya mamoja (witiri) kwa uchache tatu na kuendelea yatakayoweza kutakatisha kilichotoka na kusafisha mahali. Ya tatu: Kuwa atakayeamka kutoka katika usingizi wa usiku asiingize kiganja chake ndani ya chombo ili atawadhe mpaka akioshe mara tatu nje ya chombo, kwani hajui ni mahali gani ulilala mkono wake, hauwezi kuaminika na kutokuwa na najisi, na huenda shetani aliuchezea na akaubebesha vitu vyenye kumdhuru mwanadamu au vyenye kuharibu maji.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ni wajibu kupandisha maji puani wakati wa udhu, nako ni: Kuingiza maji puani kwa njia ya pumzi, na pia ni wajibu kuyapenga, nako ni: Kuyatoa maji puani kwa njia ya pumzi.
  2. Inapendeza kupenga kwa witiri.
  3. Ni sheria kuosha mikono miwili baada ya kutoka usingizini mara tatu.