1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Alichinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kondoo wawili wazuri weupe wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akasema, Bismillahi Allaahu Akbar, na akaweka mguu wake ubavuni mwao

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ:
ضَحَّى النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ أَقْرَنَيْنِ، ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ، وَسَمَّى وَكَبَّرَ، وَوَضَعَ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا.

Imepokelewa kutoka kwa Anas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake- amesema:
Alichinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake kondoo wawili wazuri weupe wenye pembe, aliwachinja kwa mkono wake, akasema, Bismillahi Allaahu Akbar, na akaweka mguu wake ubavuni mwao.

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 5565

Ufafanuzi

Ameeleza Anasi radhi za Allah ziwe juu yake kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alichinja kwa mkono wake siku ya Idil Adh-haa kondoo wawili madume wenye mapembe, weupe wenye mchanganyiko na weusi, na akasema: Bismillaahi wallaahu Akbaru, na akaweka mguu wake katika shingo zao.

Katika Faida za Hadithi

  1. Sheria ya kuchinja siku ya Idi kubwa (Adh-ha), na waislamu wote wamekubaliana hilo.
  2. Kilichobora zaidi ni kuwa kichinjwa kiwe cha aina hii aliyochinja Mtume rehema na amani ziwe juu yake; kwa muonekano wake mzuri lakini pia mafuta yake na nyama yake nzuri.
  3. Amesema Imam Nawawi: Hapa kuna sunna ya mtu asimamie mwenyewe kuchinja kichinjwa chake cha udhuhia, na wala asimuwakilishe yeyote ila kwa udhuru, na hapo pia ni sunna ashuhudie kichinjwa chake, na ikiwa atamuweka muislamu kwa niaba yake itafaa kwa itifaki ya wanachuoni.
  4. Amesema bin Hajari: Na hapa kuna sunna ya kutoa takbira (Allaahu Akbaru) pamoja na kumtaja Mwenyezi Mungu (Bismillaah) wakati wa kuchinja, na kuweka mguu katika weupe wa shingo wa kulia wa mnyama, na wamekubaliana wanachuoni kuwa ubavu wake unakuwa upande wa kushoto ataweka mguu wake wa kulia ili iwe rahisi kumchinja wakati wa kuchukua kisu kwa mkono wa kulia na kukamata kichwa chake kwa mkono wake wa kulia
  5. Ni sunna kichinjwa cha udh-hiya kiwe na pembe na inafaa pia kwa kinginecho.

Kuonyesha Tafsiri

53 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية