+ -

عَنْ سَعْدِ بْنِ أَبِي وَقَّاصٍ رضي الله عنه عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ قَالَ:
«مَنْ قَالَ حِينَ يَسْمَعُ الْمُؤَذِّنَ أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ، رَضِيتُ بِاللهِ رَبًّا وَبِمُحَمَّدٍ رَسُولًا، وَبِالْإِسْلَامِ دِينًا، غُفِرَ لَهُ ذَنْبُهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 386]
المزيــد ...

Kutoka kwa Sa'd Bin Abi Waqaas Allah amridhie kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Atakayesema wakati anamsikia muadhini: Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika nakuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake, nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ni Mola wangu na Muhammadi kuwa ni Mtume na Uislamu kuwa ni dini, atasamehewa dhambi zake".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 386]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema wakati akimsikia muadhini "Ninashuhudia kuwa hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiye na mshirika wake", Yaani: Nina kiri na kukubali na ninatoa habari kuwa hakuna muabudiwa wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kila mwenye kuabudiwa kinyume na yeye ni batili, "Na kuwa Muhammadi ni mja wake na ni Mtume wake" Yaani: Yeye ni mja wala haabudiwi, na ni Mjumbe wake haongopi, "Nimeridhia kuwa Mwenyezi Mungu ndiye Mola wangu Mlezi" Yaani: Kwa ulezi wake na uungu wake na majina yake na sifa zake, "Na Muhammadi kuwa ni Mtume" Yaani: Kwa yote aliyotumwa kwayo, na akatufikishia, "Na Uislamu" Yaani: Kwa hukumu zote za Uislamu ikiwemo maamrisho na makatazo, "Dini" Yaani: Kwa itikadi na kutii, "Atasamehewa dhambi zake" Yaani: Katika dhambi ndogo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuirudia rudia dua hii wakati wa kusikia adhana ni miongoni mwa mambo yanayofuta madhambi.