عَن ابنِ عباسٍ رضي الله عنهما أنَّ رسولَ اللهِ صلي الله عليه وسلم قال:
«لَو يُعطَى النّاسُ بدَعواهُم لادَّعَى رِجالٌ أموالَ قَومٍ ودِماءَهُم، ولَكِنَّ البَيِّنَةَ على المُدَّعِى، واليَمينَ على مَن أنكَرَ».
[صحيح] - [رواه البيهقي] - [السنن الكبرى للبيهقي: 21243]
المزيــد ...
Na imepokelewa kutoka kwa bin Abbas -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na baba yake -kwamba Mtume wa Mweyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Laiti wangepewa watu yote wanayodai basi kuna watu wangedai mali za wenzao na damu zao, lakini ushahidi ni kwa mwenye kudai na kiapo ni kwa mwenye kukanusha".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Albayhaqy] - [السنن الكبرى للبيهقي - 21243]
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa lau watu wangelipwa kwa msingi wa madai yao tu, bila ya ushahidi wala vielelezo, basi watu watadai mali na damu za watu wengine, lakini mwenye kudai lazima awasilishe alama na ushahidi wa kile anachodai, ikiwa hana ushahidi basi madai hayo yanawasilishwa kwa mshitakiwa, na akikanusha ni lazima aape na kuachiliwa.