+ -

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لَا صَلَاةَ لِمَنْ لَمْ يَقْرَأْ بِفَاتِحَةِ الكِتَابِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 756]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ubaada bin Swaamit -Radhi za Allah ziwe juu yake- hakika Mtume -Rehema na amani za Allah ziwe juu yake alisema:
"Hana swala yeyote ambaye hakusoma sura kifunguzi cha kitabu (suratul faatiha)".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 756]

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa sala haikubaliki isipokuwa kwa kusoma suratul Fatiha, nayo ni nguzo miongoni mwa nguzo za swala, katika kila rakaa.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية التشيكية Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Haikubaliki kusoma sura isiyokuwa suratul Fatiha ikiwa ana uwezo wa kuisoma.
  2. Kuharibika kwa rakaa ambayo haikusomwa ndani yake suratul fatiha, kwa mwenye kufanya kusudi na mjinga na aliyesahau; kwa sababu ni nguzo, na nguzo huwa hazidondoki kwa hali yoyote ile.
  3. Kisoma cha Suratul Fatiha kinaondoka kwa maamuma anapomkuta imam karukuu.