عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بِن مَسْعُودٍ رضي الله عنه قَالَ:
سَأَلْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: أَيُّ العَمَلِ أَحَبُّ إِلَى اللَّهِ؟ قَالَ: «الصَّلاَةُ عَلَى وَقْتِهَا»، قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «ثُمَّ بِرُّ الوَالِدَيْنِ» قَالَ: ثُمَّ أَيٌّ؟ قَالَ: «الجِهَادُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ» قَالَ: حَدَّثَنِي بِهِنَّ، وَلَوِ اسْتَزَدْتُهُ لَزَادَنِي.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 527]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Abdullahi Bin Masoud -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Nilimuuliza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inayopendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Ni swala kwa wakati wake", Akasema: Kisha ipi? Akasema: "Kisha wema kwa wazazi wawili" Akasema: "Kisha ipi? "Akasema: "Kupigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu" Akasema: Alinihadithia mambo hayo, na lau ningemtaka ziada angenizidishia.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 527]
Aliulizwa Mtume Rehema na amani ziwe juu yake: Ni amali ipi inapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu?. Akasema: Ni swala za faradhi katika wakati wake uliopangwa na sheria, Kisha wema kwa wazazi wawili, kwa kuwafanyia wema, na kusimamia haki zao, na kuacha kuwaasi, kisha Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya kunyanyua neno la Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuitetea dini ya Uislamu na waislamu, na kudhihirisha alama zake, na hii inakuwa kwa nafsi na mali.
Akasema bin Masoud Radhi za Allah ziwe juu yake: Alinieleza amali hizi; na lau kama ningelimwambia: Kisha ipi? Basi angenizidishia.