عَنْ أَبِي ذَرٍّ، جُنْدُبِ بْنِ جُنَادَةَ، وَأَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ، مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«اتَّقِ اللَّهَ حَيْثُمَا كُنْت، وَأَتْبِعْ السَّيِّئَةَ الْحَسَنَةَ تَمْحُهَا، وَخَالِقْ النَّاسَ بِخُلُقٍ حَسَنٍ».
[قال الترمذي: حديث حسن] - [رواه الترمذي] - [الأربعون النووية: 18]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Dharri, Jundubi bin Junada, na Abuu Abdulrahman, Muadhi bin Jabali radhi za Allah ziwe juu yao kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Mche Mwenyezi Mungu popote ulipo, na ovu lifuatishe jema litalifuta, na ishi na watu kwa tabia njema"
[قال الترمذي: حديث حسن] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy] - [الأربعون النووية - 18]
Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake mambo matatu: La kwanza: Kumuogopa Mwenyezi Mungu na hii inakuwa kwa kutekeleza wajibu, na kuacha maharamisho, katika kila mahali na nyakati na hali, katika siri na wazi, na wakati wa afya na balaa na mengineyo. La pili: Ukiangukia katika ovu, basi fanya baada yake jambo jema kama swala na sadaka na wema na kuunga udugu na toba na mengineyo, kwani hayo hufuta madhambi. La tatu: Ishi na watu kwa tabia njema, kama kutabasamu katika nyuso zao, na upole na ulaini na kutenda wema na kuacha maudhi.