+ -

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمِنينَ رَضِيَ اللهُ عَنْهَا:
كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَجْتَهِدُ فِي الْعَشْرِ الْأَوَاخِرِ مَا لَا يَجْتَهِدُ فِي غَيْرِهِ.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1175]
المزيــد ...

Imenukuliwa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akijitahidi katika siku kumi za mwisho, kwa namna ambayo hakujitahidi katika siku zingine.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1175]

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake zinapokuja siku kumi za mwisho wa ramadhani anajitahidi ndani yake kwa kufanya ibada na utiifu, na akipitiliza katika kufanya aina mbalimbali za kheri na aina za wema na ibada zaidi kuliko namna anavyojitahidi katika siku zingine; na hii ni kwa sababu ya utukufu na fadhila za siku hizi, na ni kwa sababu ya kuitafuta Lailatul Qadri (usiku wa cheo).

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Thai Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية النيبالية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Himizo la kukithirisha kutenda wema na aina mbalimbali za ibada ndani ya mwezi wa Ramadhani kwa ujumla na hasa hasa siku kumi za mwisho.
  2. Siku kumi za mwisho wa Ramadhani zinaanzia usiku wa tarehe ishirini na moja mpaka mwisho wa mwezi.
  3. Ni sunna kufaidika na nyakati bora kwa ibada.